Jumuiya daima imekuwa nguvu kuu ya Tor. tumeunda Programu ya Uanachama ya Tor Project. Lengo letu ni kujenga uhusiano thabiti kati ya shirika letu lisilo la faida na sekta binafsi ambazo hutumia teknolojia yetu au wanataka kuunga mkono malengo yetu.

Kuwa mwanachama

Jiunge na Programu ya Uanachama ya Tor Project na uonyeshe kujitoa kwako katika faragha mtandaoni na kuwa unajihusisha zaidi katika jamii ya Tor community. Tuandikie barua pepe kupitia giving@torproject.org ili kuanza.

Washirika wa Shallot Onion

Mullvad VPN

"Kuchangia katika jamii na mashirika ambayo yanajitahidi kweli kuboresha faragha na uadilifu mtandaoni ni muhimu kwa Mullvad. Kwa bahati mbaya, ni machache sana. Wale wanaoelewa faragha, wanafanya kazi kwa bidii kuboresha uzuiaji wa fingerprinting na kulinda watumiaji dhidi ya mashambulizi ya hali ya juu zaidi ni machache hata zaidi. Tunaamini kwamba Tor project ni moja ya mashirika hayo. Tunashiriki maadili yao linapokuja suala la haki za binadamu, uhuru wa kujieleza, kupinga udhibiti wa mtandao na faragha mtandaoni."

Wanachama wa Mtandaoni wa Vidalia

Onyesha kuunga mkono kwako kwa faragha mntandaoni

Taaisis yako ikijiunga na programu ya uwanachama yaTor Project’s, unaonyesha kujitoa kwako katika faragha mtandaoni na kusaidia Tor ikuwe na kwenda kwa kasi katika jamii. Matokeo yake, unakuwa sehemu ya karibu ya jamii yetu ukiwa na manufaa makubwa matatu: Kupata huduma ya kundi la ushauri wa Onion kusaidia kujumuisha Tor katika bidhaa zako, kuhusishwa katika majadiliano na mikutano maalumu na kikosi cha Tor Project kujua nini kinaandaliwa kutoka Tor, na kutangazwa uanachama wako katika umma. Kama umependa kuwa mwanachama, tafadhali wasiliana nasi kupitiagiving@torproject.org.

Madaraja ya uwanachama

Madaraja ya uwanachama hutofautiana na viwango vyao katika kuikuza katika jamii. Haijalishi kiwango cha mchango wako, wanachama hupokea manufaa sawa: kupata huduma ya kundi la ushauri wa Onion kusaidia kujumuisha Tor katika miradi yako kujumuisha katika majibizano na vikao jumuishi na kikosi cha Tor Project. Katika Tor, tunazipenda onions zote, lakini shallots ni bora zaidi!

Mshirika wa Shallot Onion

≥$100,000 per year

Nembo ya taasisi yako, iliyounganishwa nyuma ya tovuti yako, ikiwa na nukuu kutoka katika taasisi yako kuhusiana na hamasa yako ya kujiunga na programu ya uanachama, vitaonekana katika kurasa yetu ya programu ya uanachama. Pia tutakuhusisha katika mitandao ya kijamii, matukio, na njia nyingine za matangazo.

Mwanachama wa Mtandaoni wa Vidalia

$50,000 - $99,999 kwa mwaka

Nembo ya taasisi yako,iliyounganishwa nyuma ya tovuti yako,inaonekana katika kurasa yetu ya programu ya uanachama. Pia tutakuhusisha katika matangazo ya mitandao ya kijamii.

Mwanachama wa Green Onion

$10,000 - $49,999 kwa mwaka

Jina la taasisi yako, Iliyounganishwa nyuma ya tovuti yako, itaonekana katika kurasa yetu ya programu ya uanachama.

Community is at the heart of the Tor Project Membership Program, and our members agree to join our community. As such, Members agree to adhere to Tor’s Code of Conduct, Social Contract, and our Statement of Values.